Bad News For Good People, Good News For Bad People (Swahili)
Special-Order Folded Tract
NOTE: This item is custom-printed to order (click for more details).
This tract is from our print-on-demand library, and is not kept in stock. Select the options below, and we will custom-print a batch just for you. Because this item is custom-printed, you can add your custom imprint to the back page at no extra cost.
- Estimated shipping date: Wednesday, December 18 (Click for more details)
- SKU:
- Discounts: Discount coupons do not apply to this item
- Format: Folded Tract
- Size: 3.5 inches x 5.5 inches
- Pages: 4
- Imprinting: Available with 3 lines of custom text
- Returns: Because this item is custom-printed to order, it cannot be returned.
Show all item details
The full text of this tract is shown below. (Do you want to print this tract in a different version than the one listed? Contact us and let us know what you're looking for—we may be able to create the alternate version for you at no charge.)
HABARI MBAYA KWA WATU WAZURI
Yesu akasema: “Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi” (Marko 2:17)
Pengine utastaajabu kujifunza ukweli kwamba ndani ya Biblia imo habari mbaya kwa watu ambao kwa kawaida wangejiweka katika kiwango cha watu wazuri. Mistari inayofuata ni mifano ya ukweli huu:
Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi (Isaya 64:6).
Hakuna mwenye haki hata mmoja; hakuna afahamuye; hakuna amtafutaye Mungu (Warumi 3:10,11).
Vitu vyote ni vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu (Waebrania 4:13).
Mungu huyatafuta tena mambo yale yaliyopita (Mhubiri 3:15).
Si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, alituokoa (Tito 3:5).
Kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehe- sabiwa haki mbele zake (Mungu) kwa matendo ya sheria (Warumi 3:20).
Mungu ... sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu (Matendo 17:30).
Msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo (Luka 13:3).
HABARI NJEMA KWA WATU WABAYA
“Kristo alikufa kwa ajili ya waovu” (Warumi 5:6)
Pengini utastaajabu vile vile kujua kwamba yapo maandiko mengine yanayothibitisha ya kuwa kuna habari njema kwa watu wabaya. Hapa ni baadhi ya maandiko hayo:
Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi (1 Timotheo 1:15).
Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi (Warumi 5:8).
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele (Yohana 3:16).
Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea (Luka 19:10).
Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako (Matendo 16:31).
Kila atakayeliita jina la Bwana ataokoka (Warumi 10:13).
Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na tuwe na amani kwa Mungu (Warumi 5:1).
Pengine wewe ni mmoja na wale ambao wana jaribu sana kwa njia ndogo au kubwa ili wawe wazuri kusudi wapate haki ya kwenda mbinguni wakifa. Huenda ikawa unatafuta “kutenda vizuri uwezavyo” au kuishi kwa kufuata “usia” unaosema, “uwatendee wengine kama vile ungependa wakutendee.” Pengine hata unaangaliwa kuwa ni mtu wa tabia nzuri na mwaminifu katika kazi ya kidini. Vitu hivi vyote ni vyema vikiwa mahali ambapo panastahili. Lakini lazima tukuambie dhahiri kwamba Biblia haina chochote kizuri kwako ila habari mbaya. Huwezi kwenda mbinguni kwa njia hiyo. “Wote wamefanya dhambi” (Warumi 3:23) nao wako chini ya hukumu ya Mungu, na hivyo basi lazima wawe na mtu wa kuwaokoa na kuwafanya kuwa wenye haki. Wenye dhambi hawawezi kujiokoa wala hawawezi kusaidia kujiokoa.
Lakini kwa upande mwingine ukijua una hatia mbele ya Mungu, nawe umepotea na bila shaka unaenda jehanamu, Biblia kwa hakika ina habari njema kwako. Yesu Kristo alikufa kwa ajili yako juu ya msalaba wa Kalvari ili upate kuokolewa. Ukipenda, kama vile ulivyo, kwa imani mtazame Yesu. Naye anakupa msamaha wa dhambi na kuwa na uhakika wa uzima wa milele.
Yesu akasema, “Ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe!” (Yohana 6:37).