The Only Way of Salvation (Swahili)
Special-Order Folded Tract
NOTE: This item is custom-printed to order (click for more details).
This tract is from our print-on-demand library, and is not kept in stock. Select the options below, and we will custom-print a batch just for you. Because this item is custom-printed, you can add your custom imprint to the back page at no extra cost.
- Estimated shipping date: Thursday, January 23 (Click for more details)
- SKU:
- Discounts: Discount coupons do not apply to this item
- Format: Folded Tract
- Size: 3.5 inches x 5.5 inches
- Pages: 4
- Imprinting: Available with 5 lines of custom text
- Returns: Because this item is custom-printed to order, it cannot be returned.
Show all item details
The full text of this tract is shown below. (Do you want to print this tract in a different version than the one listed? Contact us and let us know what you're looking for—we may be able to create the alternate version for you at no charge.)
Kuna dini nyingi tofauti ulimwenguni, lakini zinaweza kugawanywa kwa urahisi kwa vikundi viwili. Kikundi kimoja kina mengi ya kusema kuhusu kumwagika kwa damu ya Yesu; kikundi kingine kinachukia hata kutajwa kwa damu hiyo. Kwa urahisi unaweza kujaribu madai ya dini za uwongo kwa jaribu hili moja: Je, wanaikataa damu ya Yesu kama ndiyo njia ya pekee ya wokovu.
Tukirudi kwa Biblia, tunapata kwamba, Biblia inaitaja damu ya Kristo kama njia ya pekee ya wokovu. Hadi wakati Kristo alimwaga damu yake juu ya msalaba, Mungu aliagiza damu ya wanyama kumwagwa. Hii ilikuwa picha ya damu ya Kristo iliyomwagika. Mara tu dhambi na laana ilipoingia ulimwenguni, kumwagika kwa damu kukaingia pia. Nguo zile ambazo Mungu alizowavalisha Adamu na Hawa nazo zilipatikana kwa njia ya damu kumwagika. Habili alikubaliwa na Mungu kwa sababu alikuja kupitia kwa dhabihu yenye damu. Kutoka kwa mwisho mmoja wa maandiko hadi mwingine, namna mtu anaweza kumjia Mungu inaonyeshwa kuwa inawezekana tu kupitia kwa damu. “Pasipo kumwaga damu, hakuna ondoleo” (Waebrania 9:22). “Damu yake Jesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote” (1 Yohana 1:7).
Je, yupo aulizaye kwa nini mambo haya yapo jinsi yalivyo? Ni kwa sababu dhambi ipo dhidi ya Mungu. Dhambi ni uasi dhidi ya Mungu. Wizi, ushahidi wa uwongo, uuaji na dhambi zote zinavunja amri za Mungu, nazo zinaenda kinyume cha Mungu.
Ni dhahiri basi kwamba, kwa sababu dhambi ipo dhidi ya Mungu, wokovu toka kwa laana ambayo dhambi ilileta juu ya mwanadamu lazima pia utoke kwa Mungu kwa njia ambayo Mungu ameweka. Mungu anayo njia moja tu ya wokovu, nayo ni kupitia damu. Haki na utakatifu wa Mungu unahitaji damu kumwagika.
Yawezekana njia fulani huenda ikaonekana nzuri kwako, katika njia hiyo, hutapata wokovu utakaokuwezesha kusimama mbele za Mungu ukiwa na amani siku ya hukumu. Kila dini ambayo imekataa damu ya Kristo itathibitishwa kuwa ni ya uwongo siku hiyo. Wafuasi wa dini kama hiyo bado watajikuta wakiwa bado katika dhambi zao, na hivyo basi chini ya hukumu.
Ili kuokoa mwenye dhambi, sharti Kristo apachukue mahali pa mwenye dhambi na kubeba hatia yake ya dhambi. Jambo hili alifanya huku akiichukua ghadhabu ya Mungu juu yake kikamilifu dhidi ya dhambi. Alimwaga damu yake huku akiteseka kwa ajili ya dhambi zetu. “Mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu” (1 Petero 3:18).
Umshukuru Mungu, mambo haya yote yamefanywa nayo yamemalizika, na msamaha unatolewa kwa kila mwenye dhambi. Mungu yupo tayari kusamehe. “Ambaye katika yeye (Bwana Yesu Kristo) tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi” (Wakolosai 1:14). Habari ya heri na utukufu kwa wenye dhambi waliopotea. Msomaji, je unaujua na kuufurahia ukweli wa ujumbe huu? Je, umewahi kukiri haja yako ya zawadi hii? Je, umewahi kuinama miguuni mwa Yesu katika toba la moyo kwa ajili ya dhambi yako ya maisha, na kumtazama kwa njia ya kumwabudu yeye, katika hali ya ukweli kwamba juu ya msalaba, Alikuwa anamwaga damu yake ya thamani kwa ajili ya wokovu wako? – J. W. N.
“Mwamini Bwana Jesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako” (Matendo 16:31).