The Best Gift (Swahili)
Special-Order Folded Tract
NOTE: This item is custom-printed to order (click for more details).
This tract is from our print-on-demand library, and is not kept in stock. Select the options below, and we will custom-print a batch just for you. Because this item is custom-printed, you can add your custom imprint to the back page at no extra cost.
- Estimated shipping date: Friday, February 14 (Click for more details)
- SKU:
- Discounts: Discount coupons do not apply to this item
- Format: Folded Tract
- Size: 3.5 inches x 5.5 inches
- Pages: 4
- Imprinting: Available with 4 lines of custom text
- Returns: Because this item is custom-printed to order, it cannot be returned.
Show all item details
The full text of this tract is shown below. (Do you want to print this tract in a different version than the one listed? Contact us and let us know what you're looking for—we may be able to create the alternate version for you at no charge.)
Mara nyingine tena ni wakati wa kupeana zawadi katika hali ya kisiri, upendo na kufikiriana huunganika ili kupanga mastaajabu ya furaha. Wakati kama huu, nyumba imejawa na matarajio makuu, hali, kitu kinachotamanika—kitu kinachohitajika kinachaguliwa kwa uangalifu, na kisha kufungwa na kufichwa hadi siku ifike. Katika haya yote, kuna ukumbusho mpya wa mpango wa milele wa upendo wa Mungu kukutana na mahitaji mahimu ya moyo wa binadamu, na kutoa ZAWADI ILIYO BORA ZAIDI ili kuuridhisha na kuufurahisha moyo wa binadamu kikamilifu. Hii ndiyo Zawadi yenye thamani isiyoweza kusemwa. Hii ni Zawadi ya Mungu ya uzima wa milele.
ZAWADI ILIYOHAIDIWA
Mara tu wazazi wetu wa kwanza walipotenda dhambi, Bwana Mungu alikuja chini katika shamba la Edeni ili kuwatafuta. Baada ya Mungu kuwaleta kwenye ungamo la dhambi, aliwapatia ahadi ya kwanza kuhusu Mkombozi atakayekuja katika hali ya mwanadamu kwa uzao wa mwanamke (Mwanzo 3:15). Miaka ilipita, maneno haya yanayomhusu Mwokozi atakayekuja yakaja yakawa dhahiri. Kwa mfano wa picha uliotolewa kwa wana wa Israeli kama Mwana kondoo bila mawaa— Dhabihu ya kumaliza hatia na kukomboa kutoka kwa uwezo wa shetani. Kupitia kwa manabii, Mungu alieleza dhahiri kabla ya wakati (1) Namna Atakayokuja: “Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli” (Isaya 7:14); na (2) Kule Ambako Angezaliwa: “Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja
atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele” (Mika 5:2). Kisha katika Luka 2:1-20, tunasoma kuhusu maandiko haya ambayo yalitimizwa usiku ule wachungaji walikuwa wakivichunga vikundi vyao vya kondoo kule malishoni, nao wakauona utukufu wa Mungu katika mawingu. Malaika aliwatokea na kueleza masikioni mwao yaliyokuwa tayari kusikiliza: “Msiogope kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.” Na kisha
ZAWADI HII IKATOLEWA.
Na “katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe wa pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye” (1 Yohana 4:9). Mtu mmoja kwa dhambi yake akaleta mauti kwa wote. Mungu kwa neema yake akaleta wokovu kwa wote kupitia kwa Mwanawe. Kwa Kalvari, Yesu “alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yetu” (Tito 2:14). Katika ufufuo, sasa amewekewa taji pamoja na utukufu na heshima katika mkono wa kiume wa Baba. Kupitia kwa ufunuo wa Neno la Mungu, na nguvu ya Roho wa Mungu, Yesu sasa anatolewa kwa watu wote —KWAKO kama ZAWADI ILIYO BORA ZAIDI. BORA ZAIDI, kwa sababu hakuna mwingine anayehitajika; BORA ZAIDI, kwa sababu hakuna mwingine anayetamanika zaidi. Yeye (Yesu) anahitajika, kwa sababu “Hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo 4:12). Yeye hutamanika kw
a sababu “Ndiye mzuri sana pia pia” (Wimbo Ulio Bora 5:16). Ingawa ni hivyo, ili upate kuwa na yeye kwa ajili ya mahitaji yako, na kisha kuwa na yeye kama furaha na tamaa ya moyo, lazima Awe
ZAWADI ILIYOPOKELEWA.
Zawadi uliyopewa haiwezi kuwa yako hadi utakapoipokea. Ndivyo ilivyo na wokovu. Imani ni mkono uliomtupu unaofikia nje ili kupokea zawadi ya Mungu ya uzima. Ni kule kuchukua zawadi ya Mungu wewe mwenyewe. Ni kuamini moyoni mwako kwamba mateso na mauti ya Kristo yalikuwa kwa ajili ya dhambi zako; na ya kwamba ufufuo wake kutoka kwa wafu ulikuwa kwa ajili ya kukufanya mwenye haki. Ni kuamini kuwa ZAWADI ILIYO BORA ZAIDI ni YAKO!
Mamilioni ya watu tayari wameipokea zawadi hii. Nao wamefanywa kuwa na shukrani milele kwa sababu ya baraka ambayo zawadi hii imewaletea. Uzima wa milele una mambo uliyo nayo sasa—nayo ni msamaha wa dhambi na amani kati yako na Mungu. Yote hayo yanapatikana katika zawadi hii yenye thamani isiyoweza kupimwa ya mwana mpendwa wa Mungu. Je, UTAMPOKEA SASA? Ukubali kwa imani kama Mwokozi wako, na msimu huu wenye kusherehekea utakuwa ni mmoja wa ile iliyo bora zaidi maishani mwako. —D. T. Johnson